Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya HispaniaCristiano Ronaldo bado anaendelea na matibabu ya kutibu jeraha lake la goti alilolipata dakika ya 23 katika mchezo wa fainali ya Euro 2016 dhidi ya Ufaransa, Ronaldoanahangaikiwa na wataalam ili aweze kurudi mapema uwanjani.
Kwa sasa Ronaldo ambaye yupo Ibiza akiendelea na matibabu yake na kupata mapumziko ya mwisho wa msimu, anaripotiwa kuwa atakosa mechi tatu za mwanzo, gazeti la Marca la Hispania linaripoti kuwa Ronaldo atakosa mechi za maandalizi ya msimu pamoja na mechi tatu za mwanzo.
Mechi atakazozikosa Ronaldo ni mchezo wa Super Cup dhidi ya Sevilla utakaochezwa August 9, michezo miwili ya Ligi Kuu Hispania dhidi ya Real Sociedad August 21 na mchezo dhidi ya Celta Vigo August 28, hivyo ataonekana uwanjani kuanzia September 11, Ronaldo alipata jeraha hilo baada ya kuchezewa faulo na Dimitri Payet.
Post a Comment