0

DAR ES SALAAMsanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ameoneshwa kustushwa kwake na taarifa za kifo cha mwanamuziki mwenye asili ya Congo Papa Wemba, huku akielezea jinsi walivyokutana siku chache zilizopita na kufanya naye collabo.diamond chainKwenye ukurasa wake wa Facebook Diamond ameelezea huzuni hiyo, huku akitoa taarifa kuwa kulikuwa na mipango mingi ya wao kufanya kazi, lakini mauti yameshafuta mipango hiyo.

“Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halafu ghafla naskia habari ya msiba…Dah! nimesikitika sana. Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndiyo mpangaji…Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka” aliandika Diamond Plutnums kwenye ukurasa wake wa facebookImage00003Msanii Papa Wemba amefariki dunia jana baada ya kuanguka akiwa jukwaani akiimba na kufariki papo hapo nchi Ivory Coast.

Post a Comment

 
Top