Viongozi wa Muungano wa CORD wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya
Raila Odinga na wafuasi wao wamekumbwa na zahama kubwa leo baada ya
polisi kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi katika jaribio la kutawanya
maandamano yao mbele ya jengo la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC
jijini Nairobi.
Muungano wa CORD umeitisha maandamano hayo ili kushinikiza maafisa wa tume hiyo ya uchaguzi wajiuzulu.
Makumi ya maafisa wa polisi walimiminwa kwenye jengo la Anniversary Towers ambamo ndimo zilimo ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya. Maafisa hao wa polisi walipewa amri moja tu ya kutoruhusu kufanyika maandamano yoyote kwenye eneo hilo. Polisi imewataka
waliopanga maandamano hayo wavunje mpango huo na badala yake watafute njia nyingine za kutatua matatizo yao. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nairobi, Japheth Koome alikuwa amesema mepama kuwa, wafuasi wa CORD hawataruhusiwa kuingia kwenye ofisi za IEBC. Polisi waliendelea
kusimama imara leo mbele ya jengo hilo wakati wafuasi wa CORD walipokuwa wanapiga firimbi na kusema "mapambano bado" nje ya jengo hilo kabla ya askari hao kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi wafuasi hao wa CORD na viongozi wao. Katika upande mwingine shughuli za tume ya IEBC ziliendelea kama kawaida, bila ya kuathiriwa na maandamano hayo.

Post a Comment