0
April 25 2016 headlines zilizopo katika mitandao ya soka Uingereza na Ujerumani ni kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark aliyewahi kuichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Nicklas Bendtner kuvunjiwa mkataba wake na klabu yake ya sasa ya Wolfsburg.
Nicklas Bendtner amevunjiwa mkataba na Wolfsburg baada ya uongozi wa klabu hiyo kutoridhishwa na mwenendo wa kinidhamu wa mchezaji huyo, Wolfsburg wamevunja mkataba na Nicklas Bendtner ambaye mkurugenzi wa michezo klabu hiyo Klaus Allofs  alinukuliwa akisema Nicklas Bendtner ni hatari kwa klabu mkataba wake umesitishwa.
f5e0330e85d24324991fecb841cb7fc8_20140924221354L_1 

“Mshambuliaji Nicklas Bendtner sio tena mchezaji wa Vfl Wolfsburg, mkataba wetu na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye mkataba wake ulikuwa unaisha June 2017 umesitishwa rasmi na klabu kutokana na kulalakupitiliza na kwenda katika timu akiwa kachelewa”

Bendtner aliondoka Arsenal 2014 baada ya kucheza kwa mkopo katika vilabu kadhaa na baadae akajiunga Wolfsburg  kwa mkataba wa miaka mitatu, Bendtner hajaichezea timu yake ya taifa wala klabu toka February 6, lakini Wolfsburg walitangaza kumfungia mwezi March kabla ya leo April 25 2016 kutangaza kuvunja nae mkataba.

Post a Comment

 
Top