Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa ustaarabu
wa Kiislamu hauwezi kutimia bila ya kuwepo kigezo cha maendeleo cha
Kiislamu.
Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo leo katika hadhara ya wanachama
wa Baraza Kuu la Kituo cha Kigezo cha Kiislamu-Kiirani cha Maendeleo.
Amesema kuwa kubuni kigezo cha maendeleo cha Kiislamu na Kiirani ni
sharti la kupatikana ustaarabu wa Kiislamu na kuongeza kuwa, ustaarabu
wa Kiislamu hauna maana ya kuvamia nchi bali una maana ya mataifa
mengine kuathirika na Uislamu kifikra.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa lengo la Mapinduzi ya Kiislamu ni kutimiza ustaarabu wa Kiislamu. Ameashiria misingi isiyokuwa sahihi na isiyofaa ya vigezo vya maendeleo na ustawi vya kimataifa na udharura wa kutolewa kigezo kipya cha Kiislamu-Kiirani cha kazi za kijihadi na kimapinduzi na kusema kuwa: Miongoni mwa masharti ya kuzalisha na kubuni kigezo cha Kiislamu- Kiirani cha maendeleo ni utumiaji uwezo utajiri na madhubuti wa vyanzo vya Kiislamu na vyuo vikuu vya kidini, kuwa na nguvu za kielimu na kisayansi, na kuanzisha mijadala na mazungumzo.
Ayatullah Khamenei amesema, kuunda serikali ya Kiislamu kuna maana ya kuanzisha serikali kwa msingi wa vigezo vya Kiislamu kikamilifu na kuongeza kuwa: Jamii ya Kiislamu haiwezi kuundika ila baada ya kuundwa serikali ya Kiislamu kikamilifu.
Amesema kuwa hatua ya mwisho katika awamu tano za malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ni kuhakikisha kunapatikana ustaarabu wa Kiislamu.
Ayatullah Khamenei amegusia pia vigezo vinavyotumiwa hivi sasa duniani na kusema: Nguzo za vigezo vya sasa vya ustawi si sahihi na zimesimama juu ya misingi ya fikra ya humanism (fikra za mrengo unaotanguliza mbele matakwa na matamanio ya mwanadamu kuliko Mwenyezi Mungu) na misingi isiyo ya mbinguni na matokeo yake hayakuweza kutimiza ahadi walizotoa kuhusu thamani na matukufu kama uhuru na uadilifu.

Post a Comment