0



“Ndiyo, Tunaogopa kwa sababu haya ni mapambano”. Ni jibu la mzee Wenger Alipoulizwa kama Arsenal inahofu juu ya kuwepo kwenye nafasi nne za juu. Arsenal ililazimishwa sare na Sunderland kwenye mchezo wa ligi kuu ya Epl na dalili sasa zinaonyesha wazi kuwa kocha huyo anahofu na nafasi ya timu yake kufuzu Uefa msimu ujao.

wenger

Arsene Wenger amekiri kwamba anahofu Arsenal haina uhakika wa kutinga nne bora baada ya sare ya 0 – 0 dhidi ya Sunderland.

Matokeo hayo yameifanya Arsenal kubakia nafasi ya nne ikiwa pointi tano mbele ya Manchester United ambao wana mchezo mmoja mkononi hali inayomfanya Wenger kuwa na hofu katika mechi zilizo mbele yao. Moja ikiwa ni dhidi ya Manchester City na nyingine dhidi ya Norwich inayohaha kujiokoa kushuka daraja.

Imekuwa kawaida ya Arsenal inapofika mwezi April inakuwa kwenye hatihati ya kukosa kushiriki Uefa japokuwa Januari inakuwa inaongoza ligi kabla ya kuporomoka mwezi Februari hadi nafasi ya pili kisha Machi nafasi ya tatu hadi sasa wako nafasi ya nne.

Post a Comment

 
Top