0


KANUMBA FEKI

Ni miaka minne tangu Steven Charles Kanumba afariki dunia, lakini kuongezeka kwa matukio ya kuendelea kufananishwa na watu walio hai kila uchwao sio kwamba duniani ni wawili wawili isipokuwa  ni tafsiri ya kwamba “Watu walimpenda, na bado wanampenda ila Mungu ndio alimpenda zaidi”.Steven KanumbaKama umeshaoina hiyo picha ikimuonesha Msanii wa Sanaa ya Maigizo nchini Dk. Cheni na Jamaa anayefananishwa na Marehemu Steven Kanumba, ni kwamba imepigwa jana (Jumapili ) mchana  Jijini Dar es salaam, kama anavyosimulia Dk. Cheni (Mahsein Awadhi) katika mahojiano  maalumu na mtembezi.com jinsi walivyokutana na jamaa huyo.

“Nimekutana nae jana yule mshikaji, nilikuwa nimeenda kula Mlimani City, sasa akaja mtu akaenda kuchukua chakula, kwa sababu ilikuwa ni bufee alipomaliza halafu akanigusa kwenye bega, “Habari yako naweza tuka kaa pamoja hapa?” aaaah! kabla sijamjibu nikapigwa na butwaa kama dakika 5 hivi nzima nashindwa kumjibu chochote, akarudia tena “Broo naweza tukakaa pamoja?” nikamjibu YES, YES tunaweza kukaa pamoja ingawa nilikuwa na hofu…” Alisimulia Dk Cheni.

Unaweza kusikiliza hapo chini mahojiano ya Dk. Cheni na www.mtembezi.com akisimulia jinsi alivyokutana na jamaa anayefananishwa na Marehemu Kanumba.

Moja ya kazi nzuri waliowahi kufanya Dk. Cheni na Steven Kanumba enzi za uhai wake ni Igizo la ” A Point Of No Return”.

drchenitz-20160425-0001

Mwaka 2006 Kanumba aliwahi kupata Tuzo ya “Muigizaji Bora wa Mwaka“, mwaka 2007 kutokana na juhudi zake kwenye Tasnia ya Filamu alifanikiwa kupata tuzo ya  “Muigizaji Bora wa Tanzania” na ilipofika mwaka 2007/2008 alipata tuzo ya “Msanii Bora wa Mwaka“ kabla ya kufikwa na umauti Aprili 7 2012.

Post a Comment

 
Top