Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hali ya usalama katika jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur si yenye kutabirika.
Aristide Nononsi, mtaalamu wa kujitegemea wa masuala ya haki za
binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema hayo baada ya kulitembelea jimbo la
Darfur.
Mtaalmu huyo wa masuala ya haki za binadamu amesema, hali ya usalama katika jimbo la Darfu sio ya kutabirika kutokana na kuweko makundi yanayobeba silaha.
Ripoti hiyo inatolewa siku chache baada ya kufanyika kura ya maoni katika jimbo la Darfur ambapo asilimia 97 ya wananchi waliamua eneo hilo la machafuko ya muda mrefu na ambalo liko magharibi mwa nchi hiyo liendelee na utaratibu wake wa sasa wa kiidara na chini ya majimbo yake matano.
Kwa muda mrefu jimbo la Darfur limekuwa likishuhudia machafuko na ukosefu wa usalama.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, watu zaidi ya laki tatu wameuawa katika machafuko ya Darfur yaliyoanza mwaka 2003 na wengine milioni mbili na nusu wamelazimika kuwa wakimbizi.
Mashirika ya utoaji misaada ya kibinadamu yamekuwa yakitahadharisha mara kwa mara kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo.

Post a Comment