0

Duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge Iran inafanyika leo 
 
Duru ya pili ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imeanza kufanyika leo asubuhi hapa nchini.

Wananchi milioni 17 waliotimiza masharti ya kupiga kura wanashiriki katika duru hii ya pili ya uchaguzi wa Bunge inayofanyika katika mikoa 21.

Vituo 15,350 vya kupigia kura vimeandaliwa kwa ajili ya zoezi hilo na uchaguzi huo ulianza mapema saa mbili asubuhi kwa majira ya hapa nchini kama ilivyopangwa.

Taarifa ya Tume ya Uchaguzi ya Iran inaeleza kuwa, zoezi hilo la duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge linaendelea vizuri.

Wagombea wapatao 136 wanachuana kuwania viti 68 vya Bunge vilivyosailia ambapo katika duru ya kwanza hakukupatina wagombea katika maeneo husika waliopata kura za kuwafanya watangazwe washindi.
Itakumbukwa kuwa, asilimia 62 ya wananchi milioni 55 waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki katika uchaguzi huo wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Kiislamu na wa tano wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu uliofanyika Februari 26 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top