0


Hukumu za mahakama US zinatishia sheria za kimataifa 
 
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kueleza kuwa, hukumu za mahakama za ndani za Marekani dhidi ya fedha na milki za wananchi wa Iran ni tishio kwa sheria za kimataifa.

katiba barua yake hiyo iliyokabidhiwa jana kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matafa na balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Dakta Muhammad Javad Zarif amesisitiza kuwa, Marekani inapaswa kuilipa Iran gharama za kuchelewesha kuipatia milki zake kutokana na siasa za kiadui za Washington dhidi ya wananchi wa taifa hili.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inapinga na haizitambui hukumu zisizo za kisheria za mahakama za Marekani dhidi ya taifa hili.

Siku ya Jumatano ya tarehe 20 mwezi huu, Mahakama Kuu ya Marekani ilipitisha uamuzi kuwa katika kuchunguza madai ya waathirika wa eti makosa ya jinai za ugaidi mahakama za nchi hiyo zinaweza kutumia mali na fedha za Iran zilizozuiliwa nchini humo ili kuwalipa fidia watu hao.

Mahakama hiyo ilisema dola bilioni mbili za Iran zilizo katika banki za Markenai zipewe familia za wanajeshi wa Marekani waliouawa mwaka 1983 katika hujuma ya bomu Beirut ambayo Iran inatuhumiwa kuhisika nayo. Iran imekana vikali kuhusika na hujuma hiyo na kusema fedha ambazo mahakama ya Marekani imezichukua ni mali ya Benki Kuu ya Iran.

Post a Comment

 
Top