0

Sheria mpya imeidhinishwa nchini Kazakhstan inayoruhusu utumiaji wa kemikali kuhasi ili kuwaadhibu watu waliopatikana na hatia ya kufanya ngono na watoto.

Hatua hiyo ni mojwapo ya sheria mpya kulinda haki za watoto.

Afisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Kazakhstani imesema kuwa visa vya watu wanaopenda kufanya ngono na watoto vimeongezeka kwa asilimia 50 mwaka uliopita.

Lakini wataalam wanasema kuwa kuhasi hakuna madhara makubwa ,hakudumu,hulazimika kurejelewa na ni ghali .

Post a Comment

 
Top