Ndege inayotumia nguvu ya miale ya
jua imeondoka mjini Cairo nchini Misri kwenda Abu Dhai katika awamu yake
ya mwisho ya safari ya kuizunguka dunia.
Akiongea na BBC, akiwa katika anga za bahari ya shamu , rubani wa ndege hiyo Bertrand Piccard, amesema kuwa ana matumaini kuwa ndege zinazotumia miale ya jua zinaweza kuwasafirisha hadi abiria 50 ndani ya kipindi cha miaka kumi.
Amesema kuwa teknolojia mpya anayoifanyia majaribio inaweza kusaidia kupunguza kwa nusu mafuta inayotumiwa kila siku.
Post a Comment