0

Paul Scholes anaamini kwamba Manchester United hawatakuwa wanatenda haki endapo watatoa kiasi cha paundi mil 92 (euro mil 110) kuinasa saini ya Paul Pogba kutoka Juventus, ada ambayo inaelezwa kuvunja rekodi ya usajili duniani.

Scholes ni shabiki mkubwa wa Pogba lakini amesema kwa bei hiyo inaaminisha kwamba uwezo wake ni sawa na Lionel Messi and Cristiano Ronaldo huku akisema haamini kwamba Mfaransa huyo ana thamani sawa na wakali hao wawili.

“Alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, Nimewahi kucheza naye mara nyingi tu,” Scholes aliwaambia wanahabari.

“Ni kweli amekuwa kwenye kiwango bora lakini bado siamini kama ana thamani ya paundi milioni 100 kwa sasa.”

“Kwa bei kama hiyo, ungehitaji mchezaji ambaye anaweza kufunga magoli zaidi ya 50 kwa msimu, kama Ronaldo au Messi, Pogba bado hajafika huko kabisa.”

Post a Comment

 
Top