Chama cha
Democtratic Alliance nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya
kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa
uamuzi kuwa alikiuka katiba.
Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma
alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka
2014 la kamtaka alipe pesa zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake
ya kibinafsi.
Nyumba ua Zuma ya Nkandla
Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo
mahakamani ili kumlazimu rais Jacob Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi
yaliofanywa na mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika na
mabadiliko yaliofanyiwa nyumba yake ya Nkandla.
Mamilioni ya
madola yalitumika katika kile kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa
usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na
zizi la ngombe
Post a Comment