Mwana wa kiongozi
wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ni miongoni mwa wanafunzi
waliojitokeza kuwania urais katika chama cha mijadala chuo cha Oxford.
Anasimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.
Mwisho wa video mamake Anselam Winnie Besigye, anaonekana na kusema “huna budi kushinda uchaguzi huu, nimekusaidia sana!”.
Babake Anslem, Dkt Kizza Besigye, amewania urais mara nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni bila mafanikio.
Anazuiliwa kwake nyumbani na maafisa wa usalama tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu tarehe 20 Februari.
Post a Comment