Kundi la haki za
kibinadamu Amnesty International limeishtumu Qatar kwa kuwafanyisha watu
kazi kwa lazima katika uwanja utakaochezewa mechi ya ufunguzi wa
michuano ya Kombe la Dunia 2022.
Pia imelishtumu shirikisho la soka duniani Fifa kwa kushindwa kuzuia dimba hilo linaloandaliwa chini ya unyanyasaji wa haki za kibinadamu.
Qatar imesema kuwa ina wasiwasi kuhusu madai hayo na kwamba itayachunguza.
Serikali ilisema kuwa maslahi ya wafanyikazi wahamiaji yanapewa kipaumbele na kusisitiza kuhusu marekebisho ya sheria za kazi nchini humo.
Mwaka uliopita taifa hilo liliahidi kufanyia marekebisho mfumo wa ''Kafala'' ambao huwazuia wafanyikazi wahamiaji kubadilisha kazi ama hata kuwacha kazi bila idhini ya mwajiri wao.
Lakini Amnesti imeonya kwamba marekebisho hayo hayataleta tofauti yoyote na kusema kwamba baadhi ya wafanyikazi ''wanakabiliwa na wakati mgumu''.
Post a Comment