0

Majaji kesho kuamua ni nani Aingie Fainali katika mashindano ya utangazaji AJTC Arusha

Baadhi ya majaji katika mashindano hayo.

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha (AJTC) Wanaendelea na mashindano ya utangazaji katika chuo hicho ambapo kesho   yata tangazwa madarasa matano yatakayoingia fainali na hatimaye siku ya ijumaa kujulikana mshindi.

MAKAMU MKUU WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA
 
 Makamu mkuu wa chuo hicho Bw.Elifuraha Samboto amewaasa wanafunzi wasishindane kwa ajili ya kupata fedha bali washindane kwa lengo la kuinua vipaji vyao.
Aidha ameongeza kuwa ili kuweza kupata ushindi ni lazima kila darasa washirikiane  na wawakilishi wao kwa pamoja ili waweze kupata ushindi.
MOJA YA WANAFUNZI WA CHUO HICHO AKIWASILISHA VIPINDI
Hata hivyo mshindi wa kwanza atapewa shillingi laki moja na nusu na kombe lenye dhamani ya shilling laki moja na nusu huku mshindi wa pili akipewa laki moja na mshindi wa tatu atajinyakulia shillingi elfu sabini na tano.

Post a Comment

 
Top