Watu wanane
wameuawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika mji wa
Galkayo, katikati mwa Somalia, mtandao wa habari wa Dhacdo.com
umeripoti.
Mshambuliaji huyo alijilipua akiwa katikati mwa hoteli za Capital naUunlaaye.
Meya wa mji huo Abdiasis Jama Guled ameambia BBC kwamba watu zaidi ya wanane wamefariki.
“Kuna watu zaidi ya wanane ambao wamefariki, na wengine wanane wameumia,” amesema.
Miongoni mwa waliofariki ni Said Ali Yusuf, mhasibu katika eneo la Mudug, Puntland
.
Kundi la al-Shabaab limekiri kuhusika.
Post a Comment