Mayweather akubali kuzichapa na Conor McGregor Juni 10, 2017
Mabondia Floyd Mayweather na Conor McGregor watapanda ulingoni Juni 10, mwaka huu wameuteua ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas kuwa shehemu. ya pambano lao.
Kila mmoja ametaja bei yake ya kupandia ulingoni kuwa dola za Kimarekani Milioni 100, ila kiuhalisia bondia McGregor atatakiwa kushusha bei ili kuhamishia ujuzi wake wa UFC katika ndondi.
Mayweather amesema rasmi amerejea ulingoni kwa ajili ya McGregor baada ya kustaafu akiwa amepigana mapambano 49 na kushinda yote rekodi sawa na ya gwiji, legendary Rocky Marciano na hilo litaitwa “Pambano la Karne”.
Post a Comment