Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Romelu Lukaku amekataa mkataba wenye faida kubwa kwake katika historia ya klabu hiyo.
Klabu ya Everton ambayo inashiriki ligi ya Uingereza ilikuwa na
matumaini kwamba mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ataongeza mkataba
mwingine wa miaka mitano inayoaminika kugharimu pauni 140,000 kwa wiki.
Agenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, Mino Raiola alisema
kuwa mteja wake alikuwa na uwezekano wa asilimia 99.9 kusaini mkataba
mpya katika uwanja wa Goodison Park.
Lakini Lukaku ameambia klabu hiyo kwamba hana mpango wa kuongeza mkataba mpya ambao umesalia miaka miwili kumalizika.
Lukaku hajaficha kuhusu mpango wake wa kutaka kusakata dimba la
vilabu bingwa Ulaya na amehusishwa na uhamisho wa kurudi katika klabu
yake ya zamani Chelsea, ambapo alijiunga na Everton kwa kitita cha pauni
milioni 28 mwaka 2014.
Ombi la mkataba wa Everton bado lipo wazi huku klabu hiyo ikisema kuwa majadiliano zaidi huenda yakapata makubaliano.
Lukaku hajakubali mkataba wowote na Everton huenda ikaitisha kitita
cha pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo aliyefunga mabao 19 msimu huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment