0
Msanii Harmorapa amewaomba wasanii wakubwa waliopo kwenye 'game' ya muziki kuacha tabia ya kuwapiga mkwanja mkubwa 'underground' wakati wanapoenda kuwaomba kufanya nao 'collabo'
Hayo yamekuja baada ya msanii huyo kuombwa pesa ya mavazi na Juma Nature kwaajili ya kufanyia ‘shooting video’ jambo ambalo kwa upande wake limemkwaza kwa namna moja ama nyingine.
“Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe”. Alisema Harmorapa kwenye kipindi cha eNewz ya EATV
Aidha Harmorapa amesema muda mwingine wasanii wakubwa wanatumia njia ya kutaka pesa ndefu ili mradi wa kwamishe kufanya kazi nao.
Kwa upande mwingine mzee wa kiki za mjini amesema mashairi aliyoyatumia katika wimbo wake amefanya kumjibu ‘dansa’ Mose Iyobo kutoka WCB kwa kile alichokifanya awali cha kumfananisha na sokwe.

Post a Comment

 
Top