1. Anachukia rushwa ,watoa rushwa wanaotaka kupata madaraka kwa kutoa
rushwa !! Watu wengi hawajiamini kiasi ya kwamba wanaona wasipotoa
rushwa wanaamini hawawezi kuchaguliwa!! Hawa wakishagawa pesa wanakuwa
wamenunua akili za watu!! Wanakuja na ka msemo kuwa tunapendwa
sana!!wanajificha ndani ya kichaka cha demokrasia maamuzi ya wengi
lazima yafuatwe!! Ukiwabana utasikia wanalia eti katiba ya chama
imebakwa!!Hawa lazima wamchukie JPM
2. Wapiga dili: wako watu kwa miaka mingi walijificha ndani ya chama kwa
lengo LA kuficha maovu yako mfano kukwepa kodi( wafanyabiashara)
,kufanya biashara haramu ,kujipatia kipato isivyohalali,nk!! Kwa sababu
alikosekana msemakweli na MTU Wa kuwakemea ndiyo maana walijificha
humo.watu hawa wanafikiri ni enzi za myaka ya 90 kwamba MTU
akipendekezwa na CCM lazima atashinda, wanafikiri CCM itatawala milele
vyovyote vile! Hawaamini katika kutenda meema ( siyo kutoa rushwa au
kupokea rushwa) ili uchaguliwe kwa njia ya haki( kidemokrasia) ! Hawa
wamekifitinisha chama kwa wananchi wakawaida!! Hawa lazima wamchulie
rais JPM
3. Wapinzani japo siyo wengi ambao ni wachumia tumbo!! Hawa pesa kwanza
uzalendo baadae,nchi baadae chama baadae,mwanachi baadae!! Wako tayari
kusema uongo na kuutetea kwa sababu wanajua watanzania tunapenda kusikia
siyo kufanya utafiti na kujiridhisha juu ya kilichosemwa na MTU huyu!!
Hili ni tatizo kubwa katika nchi maskini kama Tanzania!! MTU akisema
kitu tunaamini hivo hivo kama mazuzu!!
Wapinzani ambao wao ni kupinga kila JPMu wanakiri huo ndiyo upinzani Wa kweli!! Hawa lazima wampinge rais JPM
4. Watu ambao walitegemea kupitishwa na chama ili wachaguliwe!! Japo
siyo wengi lakini nao wanaweza kumchukia rais! Huko nyuma watu waliacha
kuamini chama wakaanza kumwamini MTU!! Hili nalo ni shida!! Sasa rais
anaposema watu waamini chama kuliko MTU( na huu ndo msingi imara) lazima
nao wamchukie rais!!
5. Kuna watu utafikiri waliajiriwa na watu ili kazi yao iwe kukosao kila
kitu kifanywacho na rais!! Hawa wanamtumikia mgombea Fulani wa
urais.Wanafanya hivyo kutaka kuwaminisha wananchi wasiyotumia akili
kufikiri kuwa JPM hafai Mara ni mkurupukaji,anaonea watu,ana double
standards katika kushugulikia waovu!! Hawa watu ni hatari kwa maendeleo
na mstakabali Wa taifa letu!!
6. Kuna watu wanataka kuendekeza ukabila na udini ndani ya taifa letu!!
Kipindi cha uchaguzi liko kabila La mbali ( silitaji) walifurahia
mgombea fulani ( simtaji).Nikijiuliza maana yake nini jameni!! Ukabila
ni hatari sana kwa Amani endelevu ya taifa!! Burundi hakuna amani kwa
sababu ya ukabila nakadhali nchini Rwanda ,Kongo,sudani kusini hakuna
Amani kwa sababu ya ukabila! MTU anayetaka kuendekeza ukabila ni
wakuchukia kama ukoma!! Hafai kuwa kiongozi wetu!!
7. Watu ambao hawakapata ajira,watu ambao wanavyeti feki,watu
waliyofukuzwa ajira, hawa lazima wamchukie JPM! Nafikiri ni muda mzuri
kwa serikali yetu kupunguza maadui Wa rais wetu kwa kutoa ajira kwa
vijana wetu waalimu ,madaktari,ma injinia nk!
Post a Comment