Hatimaye
 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha 
Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema baada ya kusota gerezani kwa zaidi 
ya miezi minne.
Mahakama
 hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja za pande zote mbili 
zilizowasilishwa mahakamani hapo leo na kuamua kuzitupitilia mbali hoja 
za upande wa serikali za kumnyima Lema dhamana.
Hatua
 hiyo imekuja ikiwa ni siku chache kupita tangu mahakama rufaa kutupilia
 mbali rufaa ya jamhuri, huku ikishangazwa na hatua ya Lema kukosa dhama
 hadi wakati huo.
Mbunge
 huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili 
wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1 ambapo nje ya
 mahakama Lema ametoa shukrani zake kwa wote waliohusika na kubainisha 
kuwa serikali haikuwa na nia njema na yeye, lakini yeye amesimama na 
Mungu.
"Ninamshukuru
 sana mwenyezi Mungu, mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa 
chama na wananchi wote waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke 
wangu, kama ningepata nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto 
wangu alifikia hatua akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na 
mimi gerezani, na akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani" Amesema Lema
Kwa
 upande wa wakili wake Peter Kibatala amesema hatimaye kazi ya kwanza ya
 kuhakikisha Lema anapata dhamana imekamilika na kwamba sasa wanajipanga
 kwa ajili ya kushughulika na kesi ya msingi.
Kwa
 niaba ya CHADEMA, Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, amelaani nguvu 
iliyotumiwa na jeshi la polisi siku ya leo ya kuwapiga, kuwakamata na 
kuwatawanya wafuasi wa chama hicho waliofika mahakamani hapo kufuatilia 
kesi ya mbunge wao, huku akitangaza kuwa kwa leo hakutakuwa na tukio 
lolote la kisiasa mpaka watakapotangaziwa tena.

Post a Comment