Timu za Yanga, na Azam FC za Dar es Salaaam, zimefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mabingwa wa Tanzania bara Yanga iliibugiza Ndanda FC Bao 2-1 kwa mbagoli ya Paul Nonga, na Kelvin Yondani, na lile la Ndanda FC likifungwa na Kigi Makasi.
Azam FC wao wameibuka na ushindi mnono wa bao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons kwa Bao 2 za Shomari Kapombe na moja la Mcha huku Bao la Prisons, la kufutia machozi lilipachikwa na Jeremiah John.
Robo Fainali ya michuano hili itakamilika Aprili 11 wakati Simba SC watakapocheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Kwa matokeo hayo Yanga na Azam fc zinaungana na Timu ya Mwadui FC ambayo ndio ilikuwa Timu ya kwanza kutinga Nusu Fainali baada kwa kuwachapa Geita Gold kwa mabao 3 -0.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) atawakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
Post a Comment