Kiungo huyo ambaye ni raia wa Ujerumani bado hajaamua kuhusu
mustakabali wake huku ikiwa imebaki miezi 15 katika mkataba wake wa
sasa, na kumekuwa na wasiwasi uliobuka kuwa anaweza kuondoka msimu huu
wa kiangazi.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, ndiye mchezaji anayelipwa zaidi
Arsenal akikunja kitita cha paundi 140,000 kwa wiki ambazo zinaongezeka
mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki huku akiongeza na bakshishi.
Arsenal wako tayari kumuongeza zaidi lakini Ozil anaonekana kama bado
hayupo tayari akifahamu kuwa anaweza kupata zaidi akienda kwingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment