0
Yatoa mafichoni silaha mpya, kutua nchini Aprili 5

Al-Ahly-vs-YangaWAPINZANI wa timu ya soka ya Yanga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly, ili kujidhatiti kuelekea katika mchezo wao wa Aprili 9, wameongeza makali katika safu yao ya

ushambuliaji baada ya kumjumuisha mchezaji wao, Amr Alsolah, ambaye aliachwa katika mchezo wa awali dhidi ya Recreativo de Libolo.

Nyota huyo alijiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne akitokea timu ya Al Shaab inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri.

Uongozi wa klabu hiyo umedai kwamba, kuongezwa kwa mchezaji huyo kutaisaidia klabu kufanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Yanga ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo, Sayed Hafeez, alisema kwamba hatua iliyofikia michuano hiyo ni ngumu hivyo klabu inalazimika kutumia silaha zao kwa ajili ya kusonga mbele.
“Mchezaji huyo atakuwa kwenye kikosi kinachoelekea nchini Tanzania kucheza mzunguko wa 16 dhidi ya Yanga.

“Hatua hiyo imekuja kutokana na ugumu uliopo katika hatua hiyo, hivyo tumeona bora tuongeze nguvu katika safu ya ushambuliaji kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa ugenini,” alisema Hafeez kupitia mtandao wa klabu hiyo.

Klabu hiyo imepanga kuanza safari yake ya kuja nchini Tanzania Aprili 5 kwa ajili ya kuyazoea mazingira.

Post a Comment

 
Top