Raia wa Misri wameeleza hasira zao mtandaoni baada ya serikali ya nchi hiyo kukabidhi visiwa viwili kwa Saudi Arabia.
Afisa wa serikali ya Misri ameambia kituo cha runinga cha ONTV kwamba uamuzi kuhusu visiwa hivyo umefanywa baada ya vikao 11 vya mazungumzo baina ya nchini hizo mbili katika muda wa miaka sita, shirika la habari la AP limeripoti.
Hatua hiyo imechukuliwa kiongozi wa Saudia Mfalme Salman akiwa kwenye ziara nadra sana nchini Misri.
Miongoni mwa mengine, Saudi Arabia imeahidi kutoa ufadhili na pia uwekezaji kwa Misri.
Wamisri wengi mtandaoni hawajafurahishwa na hatua hiyo.
Wanasema hiyo imeonesha udhaifu wa taifa lao na ni kana kwamba visiwa hivyo vimeuzwa.
Mwandishi wa tashtiti Bassem Youssef amekosoa serikali kwenye Twitter akisema Rais Abdul Fattah al-Sisi amepiga mnada visiwa hivyo.
Wengine wanasema hatua hiyo inonesha Rais Sisi hana uwezo na kuongoza na huenda hata ikawa ukiukaji wa katiba.
Raia wa Saudi Arabia hata hivyo wamefurahia sana hatua hiyo na wanajivunia visiwa hivyo vyao vipya mtandaoni.
Post a Comment