Gari la moshi la
dharura lililobeba lita nusu milioni ya maji inatarajiwa kuwasili
Magharibi mwa India kukata kiu ya wenyeji wa eneo hilo lililokumbwa na
ukame.
Hilo ndilo treni la kwanza kati ya mia zilizopangwa kupeleka maji Magharibi mwa India.
Mabehewa 100 ya maji yatasafirishwa umbali wa kilomita 300 hadi Latur katika jimbo la Maharashtra Kusini.
Jimbo hilo linakumbwa na ukame mbaya sana katika kipindi cha karne moja iliyopita.
Mabwawa ya maji yaliyokuwa yanategemewa kwa uhifadhi wa maji yamekauka baada ya ukosefu wa mvua kwa kipindi kirefu.
Ukame huo umesababisha hata hospitali katika eneo hilo la Kusini kuahirisha operesheni ya wagonjwa kwa sababu ya uhaba wa maji.
Post a Comment