0




obamaRAIS wa Marekani, Barack Obama, amekutana na baadhi ya wasanii wa nchini humo kwa ajili ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.

Wasanii waliopewa mwaliko huo ni pamoja na Nicki Minaj, Pusha T, Rick Ross, Busta Rhymes,

Common, J. Cole, Alicia Keys na wengine wengi, walipokutana na rais huyo walijadili namna watakavyopambana na matumizi ya dawa za kulevya.

Obama aliwataka wasanii hao watumie uwezo wao kuandika kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa kuzuia utumiaji na uuzaji wa dawa hizo.

Kupitia akaunti ya Instagram, Minaj alidai kwamba ana furaha kubwa kukutana na Rais huyo na kujadili suala hilo.

“Rais anaamini kuwa wasanii tunaweza kufikisha ujumbe kwa watu wengi wanaotuzunguka, kwa upande wangu nina furaha kwa kupata mwaliko Ikulu,” aliandika Minaj.

Post a Comment

 
Top