0

Baraka Da Prince

BAADA ya kutumbukia katika mapenzi ya mwanadada, Najma, mkali wa wimbo wa ‘Siwezi’, Baraka Da Prince yupo mbioni kuachia wimbo mpya aliouita ‘Nisamehe’.

Da Prince alisema anatarajia kuachia wimbo huoi Mei mwaka huu akiamini ni muda mwafaka kutoa wimbo huo baada ya wimbo wa ‘Siwezi’ kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.

Katika wimbo huo, Da Prince amemshirikisha msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba, aliyeutendea vyema wimbo wa kushirikishwa wa wasanii wa Kenya, Sauti Soul, katika wimbo wa ‘Unconditionally Bae’.

“Ali Kiba namkubali sana na kwa sasa ndiye aliye katika ratiba yangu hivyo ni muda sahihi wa kufanya naye ngoma yangu mpya,” alisema Da Prince.

Da Prince alisema kwa sasa hawezi kuelezea maudhui ya jina la wimbo wake huo anaotarajia kuuachia kwa kuwa ni mapema kwake na ataweka wazi kabla ya kuuzindua mwezi huo.

Post a Comment

 
Top