0


Mbwana Samatta amejitengenezea rekodi yake mpya kwenye maisha yake ya soka. Mchezaji huyo amefanikiwa kuingia kwenye timu bora ya wiki ya Europa League.

 Samatta ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kufanikiwa kufunga magoli mawili kati ya ushindi wa mabao 5-2 ambao KRC Genk walifanikiwa kuupata usiku wa Alhamisi hii dhidi ya KAA Gent.

 Kwenye orodha hiyo Samatta ameungana na wachezaji wengine 10 akiwemo Henrikh Mekhitarian wa Manchester United na Malinovskiy na Pozuelo (wote kutoka Genk).

Post a Comment

 
Top