0


Msanii mkali wa muziki, Ommy Dimpoz amesema haumizwi kichwa na kauli mbalimbali za mashabiki wake wa kwenye mitandao ya kijamii ambao wanadai kuwa anajipamba kuzidi.

Akizungumza katika kipindi cha Sporah Show cha Clouds TV, Ommy amesema yeye haumizwi na kauli hizo kwa kuwa anajijua yeye ni mwanaume wa aina gani.

“Ndo nasema haya maneno ya kwenye mitandao mimi hayaniathiri,” alisema Ommy Dimpoz.

“Mimi siwezi sema nipo tofauti na wanaume wengine, mimi nipo kawaida. Kwahiyo suala la kujipenda linaendana na hobby, kwa mfano kuna wanaume wanafanya vitu nasema no, huwezi mwanaume ukafikia kufanya hivi,” aliongeza Ommy Dimpoz.

Muimbaji huyo wa wimbo ‘Achia Body’, amesema swala la muonekano wake linamfanya achukue muda mrefu kujiandaa ili aweze kwenda sehemu.

Post a Comment

 
Top