Mganga huyo, Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anatuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 20, na kumsababishia maumivu makali.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma SACP Fredinandi Mtui alisema, mganga huyo alifanya tukio hilo, Mei 15 majira ya saa tano asubuhi.
Inadaiwa kuwa msichana alifika nyumbani kwa mganga huyo akiwa na lengo la kutibiwa masikio lakini mganga alimwambia ili dawa hiyo ifanye kazi ni lazima afanye naye mapenzi kwanza.
“Alimrubuni kuwa dawa ya sikio ili ifanye kazi inatakiwa afanye tendo la ngono na kwa ujanja huo , alimbaka msichana huyo,” alisema Kamanda.
Kamanda Mtui alisema kwa sasa mganga huyo anashilikiwa na polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote.
Katika tukio jingine, mkazi wa Mvinza, kata ya Kagera Nkanda Josephine Ntahukisiga (42) ambaye ni mkulima amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya nyumba ya baba yake kwa kutumia shuka.
Tukio hilo lililotokea Mei 14, 2015 inaelezwa kuwa Ntahukisiga alivizia ndugu zake wakiwa wamelala ndipo alipoenda sebuleni na kujinyonga kwa kutumia shuka kwa kulifunga juu ya dari.
Kwa mujibu wa baba wa marehemu, Andrew Ntahukisiga alisema marehemu alikuwa na msongo wa mawazo tangu watoto wake walipofariki kwa ajali ya moto mwaka 2015.
Post a Comment