Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad
Zarif amesisitiza kuhusu ulazima wa kuwepo umoja miongoni mwa makundi
yote ya Palestina.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Irana amesema leo umoja wa makundi yote ya Kipalestina ni jambo la dharura. Aidha amesisitiza kuwa, lengo la ulimwengu wa Kiislamu na makundi ya kupignia ukombozi wa Palestina ni kuondoa hatari ya utawala wa Kizayuni.
Zarifa amesema kadhia ya Palestiina ni kadhia muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa, ni jambo lilislokubalika kudunisha hatari ya utawala wa Kizayuni.
Katibu Mkuu wa Jihad Islami kwa upande wake amewasilisha ripoti kuhusu hali ya mambo Palestina na eneo pamoja na nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika utatuzi wa matatizo ya eneo.
Post a Comment