Mvulana mmoja nchini Australia alifanikiwa kujitambulisha kama waziri mkuu wa nchi hiyo kwa siku mbili mwishoni mwa wiki.
LakiniOrley Fenelon, mwenye umri wa miaka 12, anayetoka mji wa Brisbane alijiweka katika tovuti ya Wikipedia kama waziri mkuu wa tano bila kutambulika.
Hata waziri mkuu wa sasa Malcolm Turnbull hakujua kwamba alikuwa ‘ameondolewa madarakani’.
Tovuti hiyo yenyewe haikugundua mabadiliko hayo.
"Mimi na marafiki zangu tulikuwa tunazungumzia kinyang’anyiro cha urais Marekani na ndipo tukapata wazo la ‘Orley kuwania wadhifa wa Waziri Mkuu’,” aliambia BBC Newsbeat.
"Niliweka hilo kwenye Instagram na baadaye nikahariri ukurasa wa orodha ya mawaziri wakuu wa Australia kwenye Wikipedia.”
Nilidhani ingegunduliwa mara moja na kufutwa. Lakini hilo halikufanyika.
"Ilifika pahali nikadhani kuna mtu angekuwa anaandika kitabu (kuhusu siasa za Australia) na anihesabu,” alisema huku akicheka.
"Nilipokuwa waziri mkuu hakuna kubwa lililotokea. Muhula wangu ulikuwa umetulia,” anatania.
Hakuna waziri mkuu aliyefanikiwa kumaliza muhula wake Australia tangu 2007.
Orley ni mwanafunzi wa darasa la saba na anasema angetaka kuwa mtu wa kuchekesha na kuchezea watu.
Lakini akifanikiwa kuwa waziri mkuu wa Australia mwaka wakati mmoja, anasema angeifanya Australia kuwa Jamhuri na kumuondoa Malkia wa Uingereza ambaye kwa sasa ndiye kiongozi wan chi.
Post a Comment