MSHAMBULIAJI wa timu
ya Atletico Madrid, Fernando Torres, ameendelea kuikumbuka kadi nyekundu
ambayo alioneshwa katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa dhidi ya Barcelona na kudai kwamba bila kadi hiyo Atletico
ingeshinda.
Katika mchezo huo
ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Nou Camp, Atletico walikuwa wa kwanza
kupata bao, lakini Barcelona walifanikiwa kupata bao la kusawazisha na
kuongeza katika ushindi wa mabao 2-1.
Bao la pili la
Atletico lilifungwa huku Atletico wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji
huyo kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu na kuoneshwa
kadi mbili za njano. Hata hivyo, Torres amedai kwamba wangeshinda mchezo
huo kama wangeendelea kuwa 11.
“Bado ninaifikiria
kadi ambayo nilioneshwa kwenye mchezo wa robo fainali kwenye Uwanja wa
Nou Camp, ninaamini tulikuwa na kila sababu ya kushinda kama
tungeendelea kuwa 11 uwanjani.
“Kadi ya kwanza ya
njano ilikuwa sahihi, lakini ya pili haikuwa sahihi, ila ndicho
kilichotokea na ninaamini mchezo wa kesho (leo) tunaweza kushinda
nyumbani,” alisema Torres.
Timu hizo zinatarajia
kushuka dimbani leo hii kwa ajili ya marudiano ambapo lazima mmoja
ayaage mashindano baada ya mchezo huo kumalizika.
Post a Comment