0


Vipo vitu ambavyo ukivisikia unakua na maswali mengi sana kichwani,katika vitu ambavyo nimekutana navyo ni pamoja na hii ya Mizizi kuota kuelekea juu kama ukuta sio chini tena kama ambavyo tumezoea kwa mimea mingine.
5Mti huu unaitwa Entandrophragma Excelsum unapatikana kwenye Msitu wa Mazumbai uliopo Bumbuli kwenye wilaya ya Lushoto kwenye mkoa wa Tanga na kizuri zaidi Msitu huu umehifadhiwa na Serikali chini ya chuo kikuu cha Sokoine kwa ajili ya watu kwenda kujifunza.
3Msitu huu wa Mazumbai nimewambiwa unasifa nyingi sana za kipekee,kwanza ni kati ya misitu michache ambayo haijaathiriwa na shughuli za kibinadamu na hii ni kutokana na ulinzi uliopo hapo pia msitu huu una aina nyingi za mimea kuliko aina za mimea inayopatikana Ulaya Magharibi.
2Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli Mh.January Makamba ni miongoni mwa Wageni waliopata nafasi ya kutembelea msitu huu.
1

Post a Comment

 
Top