Jaxon Buell alizaliwa August 27 2014 huko Birmingham, Uingereza akiwa hana sehemu kubwa ya fuvu la kichwa pamoja na ubongo.
Madaktari waliligundua tatizo la huyu mtoto tangu kipindi ambacho bado hajazaliwa, Brandon na Brittany
ambao ni wazazi wake walishauriwa na Madaktari kwamba ni bora ujauzito
wake ukatolewa… wao hawakukubali, kingine kikafuatia kwamba hata
akizaliwa,hatokuwa na maisha marefu atafarariki kutokana na ukubwa wa
tatizo lake.
Baada
ya miezi mingi kupita akiwa anafanyiwa uchunguzi na madaktari
waligundua kuwa hakuna kinga yoyote itakayomsaidia kuendelea kuishi
lakini wazazi wake hawakukata tamaa na walifanya kila jitihada
kuhakikisha mtoto wao anaendelea kuishi.
Wazazi wa Jaxon, Brandon na Brittany pamoja na mtoto wao wakiwa na nyuso za furaha
Post a Comment