0

                   Mwasiti Almasi
 
Nyota wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi amesema wimbo wake mpya alioupa jina la 'Sema Naye' unafanya vizuri sehemu mbalimbali mikoani tofauti na ilivyo jijini Dar es Salaam.
 
Mwasiti alisema kuwa sababu kubwa ya wimbo huo kutopokelewa vizuri Dar es Salaam ni mazoea ya baadhi ya mashabiki kuona msanii akifanya vitu vyake bila kubadilika.
 
"Katika wimbo wa Sema Naye nimeimba tofauti na vile ambavyo mashabiki wamezoea na hilo ni jambo la kawaida kwa msanii anayejua kile anachokifanya, lakini bahati wachache hawakunielewa," alisema Mwasiti.
 
Msanii huyo aliiambia Nipashe kuwa mashabiki wamezoea kumsikia akiimba muziki wa kizazi kipya kwa mtindo mmoja, lakini katika wimbo wake mpya amefanya vitu vyake vipya ambavyo vimeonekana kuwa vigeni kwao.
 
Hiyo ndio sababu kubwa ambayo ninaweza kusema kuwa imefanya hapa Dar es Salaam nikutane na changamoto za wimbo wangu kutopokelewa vizuri, lakini bahati nzuri unasikika sana mikoani," alisema.
 
Mwasiti ni miongoni wasanii nyota walioibuliwa na Nyumba ya Vipaji nchini (THT) na amekuwa akifanya vizuri kwenye nyimbo zake mbalimbali zilizomfanya awe na jina katika muziki wa kizazi kipya.

Post a Comment

 
Top