Kundi la Muziki wa taarabu Mashauzi Classic
Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid maarufu kama Suma alisema jana kuwa Kundi la Mashauzi Classic lilitua jana kutoka Muscat, Oman lililokwenda kwa ajili ya kufanya maonyesho kadhaa.
Suma alisema, itakuwa mara ya kwanza kwa bendi hizo mbili kupiga pamoja katika ukumbi huo wa Mango Garden.
Alisema Isha Mashauzi pia atatambulisha nyimbo wake mpya zijulikanayo kama “Kismat” na “Jiamini”.
Pia ameahidi kupiga nyimbo zake zote maarufu na zinazopendwa na
mashabiki wa taarabu nchini, zikiwamo “Sura Surambi” na “Nimpe Nani”.
Naye mratibu wa onyesho hilo, Joseph Kapinga alisema katika
mpambano huo, Twanga Pepeta watatambulisha nyimbo zao mpya kama 'Mtu
Makini' utunzi wa rapa Fagason na 'Twanga Kwanza' utunzi wake Roggart
Hegga Katapila.
Alisema pia Fugason ataendeleza kutambulisha rapu yake mpya ijulikanayo kama “Banjuka”.
Pia bendi hiyo pia itawatambulisha wanenguaji wake wapya Kama Super K na Chiku Kasika.
Onyesho hilo limeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment chini
ya udhamini wa Konyagi, LeteRaha, Fredito Entertainment, Saluti5 na CXC
Africa.
Post a Comment