Ule ujumbe wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kuwa ameteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa msemaji msaidizi wa Ikulu imezua gumzo kubwa.
Ujumbe huo umesambaa kwenye mitandao kibao ya kijamii hasa Whatsapp, Instagram na Facebook ukionyesha Muro atakuwa msaidizi wa Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Ikulu chini ya Gerson Msigwa.
Hata hivyo, Muro amezungumza na SALEHJEMBE usiku huu na kuthibitisha kuwa taarifa hizo ni uzushi mtupu.
“Hakika ni uzushi, kwanza ile akaunti ya Twitter iliyoanza kusambaza si yangu,” alisema Muro ambaye tayari TFF imetangaza kumfungia huku ikiwa haijatoa hukumu.
UJUMBE ULIVYO…
USIEMPENDA KAJA!!!!!!!!
BREAKING NEWS
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemthibitisha Ndg Geryson Msigwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu huku msaidizi wake akiwa ni aliyekuwa msemaji wa Klabu ya soka ya Yanga Ndg Jerry Cornel Muro.

Post a Comment