Mulipuko wa homa ya
manjano umewaua watu 21 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Kwa
mujibu wa Shirika la Afya Duniani{WHO}, homa hii imetoka katika nchi
jirani ya Angola.
Taarifa ya WHO inasema vifo hivyo vilitokea
mwezi Machi huku kukiwa na visa vingine 151. Kuna hofu huenda mulipuko
huu ukasambaa zaidi. Homa hii ya manjano imewaua watu 225 nchini Angola
na kuwaambukiza wengine 1,600.
Homa ya manjano huambukizwa na mbu aina ya {Aedes aegypti}
WHO imeongeza kwamba maafisa wa DRC wameweka vituo
vya dharura kushughilikia mulipuko huo.Aidha raia wanaosafiri nchini
Angola watapewa chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Homa hii husababisha kuvuja
damu na figo kushindwa kufanya kazi.
Inaambukizwa na aina ya mbu
{Aedes aegypti}. Maeneo yaliyo kwenye hatari ya Homa ya manjano ni
pamoja na Bara Afrika na Amerika Kusini.
Post a Comment