Wapiganaji wa Al shabaab wameendeelea kuwalenga wanajeshi wa serikali na wale wa kigeni nchini Somalia
Jeshi la Marekani
limesema kwamba lilitekeleza mashambulio ya anga nchini Somalia na
kuwaua wapiganaji 12 wa kundi la Al Shabaab. Idara ya ulinzi imesema
wapiganaji hao walitishia usalama wa maafisa wa Marekani ambao
wanasaidia wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Wiki jana idara ya ulinzi ya Marekani ilisema kiongozi mmoja wa Al Shabaab Hassan Ai Dhoore alikua ameuawa kwenye shambulio la ndege isiyo na rubani. Wapiganaji hao wamekua wakitekeleza mashambulizi makali dhidi ya maafisa wa serikali ya Somalia, wanajeshi wa kigeni sawa na kulenga hoteli na migahawa katika mji mkuu Mogadishu.
Post a Comment