Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kufuatia maandamano ya wanafunzi
Chuo Kikuu cha
Nairobi kimewafukuza wanafunzi 139 zaidi kwa kushiriki mgomo
uliosababisha uharibifu mkubwa wa mali. Wanafunzi hao walitakiwa
kuchukua barua za kufukuzwa kutoka kwa msajili wa wanafunzi ifikapo
Ijumaa ya wiki hii.
Naibu Chansela wa Chuo hicho Profesa Peter
Mbithi amesema hii ni moja wapo ya hatua za kinidhamu dhidi ya wanafunzi
walioongoza mgomo huo. Kwa sasa Chuo hicho kimefungwa. Jumanne wiki hii
wanafunzi 62 walifukuzwa akiwemo Mike Jacobs mgombea wa wadhifa wa
Mwenyekiti wa chama cha wanafunzi{SONU}.
Wanafunzi walilalamikia matokeo ya uchaguzi wa chama cha wanafunzi{SONU}
Jacobs alikua mpinzani wa mwenyekiti wa sasa Babu
Owino. Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi baada ya kupata silaha
ikiwemo visu vilivyokua na damu hali inayozua hofu ya kuwepo magenge ya
uhalifu ndani ya Chuo hicho.
Post a Comment