Kampuni ya vinywaji
vya Coca Cola imelazimika kulifanyia mabadiliko tangazo lake la
biashara linalofahamika kama "Taste the feeling" kufuatia kuingiliwa
kati na bodi inayodhibiti filamu nchini Kenya.
Mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu ya bodi hiyo nchi Kenya Ezekiel Mutua, alisema kuwa tangazo hilo lilikosolewa na umma kutokana na picha za kubusiana ambazo zinatajwa kuwa za kukiuka maadili ya kijamii.
Mutua amesema kuwa baada ya kufanya mkutano na meneja wa Coca Cola nchini Kenya Nicholas Mruthu , kampuni hiyo imekubali kuleta tangazo lingine lisilo na picha kama hizo.
Bodi hiyo pia imeonya makampuni ikiyataka yaheshimu maadili ya familia kutokana na kile yanayojumuisha kwenye matangazo ya biashara na muda ambao matangazo hayo yanapeperushwa .
Post a Comment