Simba ambaye
alitoroka mara mbili kutoka kwa mbuga ya wanyamapori nchini Afrika
Kusini atapewa makao mpya ambapo ataishi na simba wawili wa kike na
kujifunza jinsi la kuwa simba imara.
Simba huyo mwenye umri wa
miaka mitatu kwa jina Sylvester aliondoka kwenye mbuga ya Karoo
magharibi mwa mji wa cape town kwa mara ya pili na uamuzi ya kumuua
ulitupiliwa mbali kutokana na malalamishi ya umma.
Simba huyo aliwaua kondoo wengi mwezi Juni
Sylvester aliyepewa jina la myama mwenye kusumbua na
maafisa wa mbuga, sasa atapelekwa kwenye mbuga ya ndovu ya Addo, katika
mkoa wa Eastern Cape ambapo ataishi na simba wawili wa kike.
Mwezi
Juni simba huyo aliwaua kondoo wengi na kusafi umbali ya kilomita 300
kabla ya kupatatika akiwa amalelala na walinzi wa mbuga.
Post a Comment