0


Iran: Dunia iungane katika vita dhidi ya ugaidi 
 
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonya kuhusu kuenea ugaidi na misimamo mikali duniani na kusema jamii ya kimataifa inapasa kushirikiana kukabiliana na uovu huo. 
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Morteza Sarmadi alipozungumza na waandishi habari baada ya Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kongamano la Maingiliano na Hatua za Kuaminiana ASIA (CICA) mjini Beijing Uchina, Ijumaa.

Ameongeza kuwa kuwa dunia inashuhudia kuongezeka ugaidi, taasubi za kimadhehebu na makudni wa wakufurishaji na hivyo kupelekea hali kuwa ngumu katika nchi nyingi hasa Mashariki ya Kati.
Sarmadiametoa wito kwa nchi za Asia kushirikiana kwani kukabiliana na ugaidi ili eneo hilo

lishuhudie amani na usalama. Aidha amebainisah azma ya Iran ya kuimarisha ushirikiano wa nchi za CICA

Post a Comment

 
Top