0


Kodivaa yawarejesha nyumbani raia wake kutoka Gabon  
 
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ivory Coast imetangaza kuwa, imewarejesha nyumbani zaidi ya raia 100 kutoka Gabon kutokana na kuwa na hali mbaya za kimaisha. 
 
Kwa mujibu wa wizara hiyo ya mashauri ya kigeni ya Kodivaa watu 127 kati ya 460 tayari wamerejea nyumbani kwa hiari kutokana na matatizo ya kimaisha. Imeongeza kuwa raia hao ambao awali waliomba kurejea nyumbani kwao, waliwasili jana na ndege maalumu ya serikali mjini Abidjan, mji mkuu wa zamani wa nchi hiyo. Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Ivory Coast

imeongeza kuwa, watu hao 127 ni pamoja na watu wazima na watoto. Tarehe tisa Machi mwaka huu, serikali ya Kodivaa ilitangaza azma yake ya kuwarejesha nyumbani raia wake 170 hadi 460 ambao wanaishi katika hali ngumu ya kimaisha nchini Gabon na Angola. Baada ya kurejea nyumbani

serikali ya Yamoussoukro ilimpatia kila mmoja wao kiwango fulani cha Frank za nchi hiyo ambazo ni sawa na dola 200 za Kimarekani pamoja na chakula.

Post a Comment

 
Top