0


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza kuundwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Sudan Kusini 
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha kuundwa serikali ya عmoja wa نitaifa nchini Sudan Kusini baada ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kuliapisha baraza jipya la mawaziri na kuzitaka pande husika zikamilishe hatua zote za kuunda taasisi za serikali hiyo ya mpito. 
 
Ban ametoa taarifa hiyo akisema kuwa amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ya mahasimu wawili Rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar ya kukubali kufanya kazi kwa pamoja na kumaliza mgogoro wa miaka kadhaa wa nchi hiyo. Amesema viongozi hao na pande zote husika

zinapaswa kuongeza juhudi za kuukamilisha mchakato mzima wa kuunda taasisi zote za serikali hiyo ya mpito. Aidha amezitaka pande hizo zikomeshe haraka uhasama baina yao. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amependekeza tume maalumu ya kusimamia zoezi hilo inayojulikana kwa kwa kifupi JMEC ambayo miongoni mwa wajumbe wake ni Rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae, na Rais wa zamani wa Mali, Alpha Omar Konare kwa ajili ya kusimamia mchakato wa amani na kuhakikisha kuwa Sudan Kusini inarejea katika usalama, utulivu na maelewano.

 Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa iendelee kusaidia juhudi za kuleta amani na kuhakikisha kuwa makublaiano ya amani ya Sudan Kusini yanatekelezwa kikamilifu. Itakumbukwa kuwa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa ya Sudan Kusini ina mawaziri 30 kutoka kwa wafuasi wa Rais Salva Kiir na wa mkuu wa zamani wa waasi, Riek Machar ambaye sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais. Riek Machar aliapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini mara baada ya kurejea mjini Juba siku ya Jumanne.

Post a Comment

 
Top