Wizara ya Mambo ya Mahakama nchini Chad imetangaza kuachiliwa huru
wachimba mgodi 103 raia wa nchi hiyo ambao walikuwa wakishikiliwa nchini
Algeria kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Wizara hiyo ya Vyombo vya Mahakama na ambaye hakutaka kutaja jina lake, wachimbamigodi hao wanaojishughulisha na uchimbaji dhahabu katika milima ya Tibesti inayoishia kaskazini mwa nchi hiyo, walitiwa mbaroni na askari wa Algeria mwaka mmoja uliopita na kuzuiliwa nchini humo kwa kipindi chote hicho. Baadhi ya duru zimesema kuwa, wachimba
migodi hao wameachiliwa huru kufuatia msamaha wa Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ambaye ameamua kuwasamehe raia hao wa Chad. Wachimbaji hao wadogowadogo wa madini kutoka Chad hupendelea sana kufanya shughuli zao katika milima ya Tibesti, na wakati mwingine wanavuka mmpaka na kuingia Niger na kufika hadi katika ardhi ya Algeria kupitia Nigeri kwa ajili ya kuchimba dhahabu kinyume cha sheria.
Post a Comment